Makafiri wote wanaombewa uongofu na si msamaha


Swali: Je, inajuzu kuwaombea du´aa ya uongofu Ahl-ul-Kitaab walio na mkataba [na waislamu]?

Jibu: Tunawaombea makafiri wote uongofu. Kuhusu uongofu tunamuombea nao kila kafiri, ni mamoja ikiwa ni watu wa Kitabu na wengineo. Kilichokatazwa ni kuwaombea msamaha. Hatuwaombei msamaha mpaka wasilimu. Hatuwaombei msamaha mayahudi, manaswara na wengineo mpaka wasilimu. Kuna tofauti kati ya msamaha na uongofu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (62) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13740
  • Imechapishwa: 16/11/2014