Makafiri kuingia msikitini

Swali: Je, inafaa kuwaruhusu manaswara, mayahudi au makafiri wengine kuingia ndani ya msikiti kuja kutembea?

Jibu: Hapana ubaya kwa kafiri kuingia msikitini ikiwa ni kwa lengo linalokubalika katika Shari´ah au jambo linaloruhusiwa. Kwa mfano akaingia kwa ajili ya kusikiliza mawaidha, kunywa maji na mfano wa hayo. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baadhi ya wajumbe wa kikafiri aliwaacha watue ndani ya msikiti wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili wawaone waswaliji, wasikilize kisomo na Khutbah yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lengo lengine alikuwa anataka kuwalingania kwa ukaribu. Isitoshe (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimfungamanisha Thumaamah bin Athaal msikitini alipoletwa kwake kama mteka. Baadaye ndipo Allaah akamwongoza na akasilimu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (08/356)
  • Imechapishwa: 25/06/2021