Majini hawawezi kumtumikia mtu mpaka na yeye awatumikie

Swali: Kuna mtu tunamjua anaswali Rakaa zote Msikitini na anaonekana kuwa na Sunnah. Lakini anadai ya kwamba majini Waislamu wanamtumikia kwa kumtibu.

Jibu: Huyu amepewa mtihani. Ni wajibu kutahadhari naye. Ni wajibu kutahadhari naye. Majini hawawezi kumtumikia mtu isipokuwa kama na yeye atawatumikia. Hawaaminiki na wala hawajulikani hata kama watadai Uislamu. Ni wajibu kutahadhari. Badala yake kinachotakiwa ni kuwanasihi, kuwaelekeza, kuwaamrisha na kuwakataza kwa kuwaambia: “Mcheni Allaah na wala msiwaudhi waja wa Allaah. Kuweni na msimamo katika Dini ya Allaah”. Ama kuwafanya kuwa ni wafanya kazi wake na kumtumikia, hapana. Haijuzu. Kwa kuwa hili ni katika aina ya kuwatumia makuhani na wapiga ramli. Kwa kuwa makuhani na wapiga ramli wanadai vitu katika mambo ya ghaibu, wanawatatiza watu na [katika kazi yao] wanatumia majini. Kadhalika watu wote wenye kazi chafu na wachawi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=14579
  • Imechapishwa: 05/05/2015