Majina ya Allaah yanayokuwa chini kwenye barabara na magazeti

Swali: Kuna magazeti mengi yanayokuwa na majina ya Allaah (´Azza wa Jall) na wakati tunapopita barabarani na kuyaona tunajihisi vibaya. Wakati mwingne tunayachukua na wakati mwingine kwenye barabara hiyo hiyo kunakuwa wanaume na hivyo tunapita na kuyaacha chini. Je, tunapata dhambi kwa hilo?

Jibu: Ndio. Unapoona Jina la Allaah, Aayah katika Qur-aan au Hadiyth ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenye barabara ni wajibu kwako kuinyanyua. Ima iweke sehemu ambayo ni safi au ichome moto. Usiiache ikachafuliwa na kutwezwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_makruf%201-10-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 24/09/2020