Majina maalum kwa Allaah ambayo haifai kwa viumbe kuitwa nayo

Swali: Je, kuna majina ambayo haifai kuitwa kwayo?

Jibu: Haifai kuitwa kwa majina ambayo ni maalum kwa Allaah kama vile ´Allaah`, ´ar-Rahmaan` (Mwingi wa huruma), ´Maalik-ul-Mulk` (Mfalme wa wafalme), ´Khaaliq-ul-Khalq` (Muumba wa viumbe), ´Rabb-ul-´Aalamiyn” (Mola wa walimwengu), ´an-Naafiy´ adh-Dhwaar` (Mwenye kunufaisha, kudhuru), ´al-Mu´twiy al-Maaniy´` (Mwenye kutoa, Mwenye kuzuia),  ´Haakim-ul-Hukkaam` (Hakimu wa mahakimu), ´Sultwaan-us-Salaatwiyn` (Mfalme wa wafalme), ´Aqdhwaa´-ul-Qudhwaat´ (Qadhiy wa maqadhiy). Haijuzu kujiita kwa majina haya. Vilevile mtu anapaswa kuepuka majina mabaya na maovu. Lililowekwa katika Shari´ah ni mtu kuchagua majina mazuri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (01) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=190884#219018
  • Imechapishwa: 03/01/2018