Majimaji yanayomtoka mwanaume au mwanamke baada ya kukoga janaba

Swali: Baada ya kukoga janaba, natokwa na kitu kama manii. Je, ni wajibu kwangu kurudi kukoga tena?

Jibu: Hapana sio wajibu, maadamu umekwishakoga manii haya hayana maana yoyote. Kwa kuwa yametoka bila ya shahawa, hukumu yake ni kama ya mkojo, hayana maana yoyote. La wajibu ambalo ni kukoga umekwishatekeleza, haidhuru kutoka kwa manii ambayo ni athari ya jimaa uliofanya. Hali kadhalika mwanaume, lau atakoga kisha yakamtoka baada ya hapo pamoja na mkojo, haidhuru hilo maadamu alikoga kwa jimaa aliofanya mwanzoni. Ama yakitoka kwa shahawa nyingi, au kwa kupapa sana, au kwa kubusu au kwa mfano wa hayo katika mambo ambayo ni sababu ya kutoka kwa manii kwa shahawa, haya yatakuwa ni manii mapya ambayo yanahitajia kukoga. Ikiwa yametoka kwa shahawa mpya; sawa ikiwa ni kwa kuangalia, kupapasa au kubusu, haya hukumu yake itakuwa ya janaba mpya. Ni juu ya yule ambaye yamemtoka akoge upya sawa ikiwa ni mwanaume au mwanamke. Ama ikiwa ni (athari ya) yaliyobaki kwa (kitendo) alichokifanya nyuma, hayadhuru na wala hayahitajii kukoga upya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 26/03/2018