Majimaji yanayomtoka mwanamke baada ya kuoga janaba

Swali: Je, majimaji yanayomtoka mwanamke baada ya kuoga janaba yanawajibisha kuoga tena au hapana?

Jibu: Hayawajibishi kuoga tena. Kuoga janaba hakuwajibiki isipokuwa kwa moja kati ya mambo mawili:

1- Jimaa. Haijalishi kitu hata kama mtu hakumwaga.

2- Kutokwa na manii hata kama mtu hakufanya jimaa.

Kukipatikana kutokwa na manii na kufanya jimaa hukumu yake inatambulika. Hukumu yake ni kwamba ni wajibu kuoga.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (38) http://binothaimeen.net/content/863
  • Imechapishwa: 28/06/2018