Swali: Mwenye kusema kuwa majibali yanatembelea katika zama zetu hizi kwa kutumia dalili maneno Yake (Ta´ala):

وَتَرَى الْجِبَالَ تَحْسَبُهَا جَامِدَةً وَهِيَ تَمُرُّ مَرَّ السَّحَابِ

“Na utaona majabali ukiyadhania yametulia thabiti nayo yanapita mpito wa mawingu.” (27:88)

Je, maneo haya yanazingatiwa ni katika kuifasiri Qur-aan kwa maoni yake?

Jibu: Ndio. Huyu ni mwongo. Anazungumza juu ya Allaah pasi na elimu. Aayah:

وَتَرَى الْجِبَالَ تَحْسَبُهَا جَامِدَةً وَهِيَ تَمُرُّ مَرَّ السَّحَابِ

“Na utaona majabali ukiyadhania yametulia thabiti nayo yanapita mpito wa mawingu.” (27:88)

hili linahusu siku ya Qiyaamah na si leo. Leo majibali ni yako imara na yamekaa kama vigingi vya ardhi.

وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ شَامِخَاتٍ

“Na Tukaweka humo milima mirefu thabiti… ” (77:27)

Iko thabiti. Je, kitu kilicho imara hutembea? Hapana, haitembei. Huku ni kuzungumza juu ya Allaah pasi na elimu na ni kufasiri Qur-aan kwa nadhariya. Qur-aan haifasiri isipokuwa kwa kutumia Qur-aan, Sunnah, maneno ya Maswahabah au maneno ya Taabi´uun. Hizi ndio njia za kufasiri Qur-aan. Qur-aan haifasiriwi kwa maoni au nadhariya kwa kuwa ni Maneno ya Allaah. Yule anayeifasiri kinyume na maana yake anazungumza juu ya Allaah pasi na elimu. Anasema kuwa Allaah anakusudia hivi ilihali ni mwenye kusema uongo katika hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (14) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-10-15.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020