Maji yanayomtoka mjamzito na wudhuu´

Swali: Je, maji yanayomtoka mwanamke kabla ya kuzaa ni najisi na yanachengua wudhuu´?

Jibu: Ndio. Ni katika damu ya uzazi. Maji yanayotoka kabla ya kuzaa ni katika mwanzo wa damu ya uzazi. Ni najisi, kwa sababu yanatoka ukeni. Aidha yanachengua wudhuu´.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (30)
  • Imechapishwa: 20/02/2022