Maji yananajisika kwa kuingiza mikono ndani yake?

Swali: Je, mwanaume akiingiza mikono yake ndani ya maji inafaa kuyatumia au hapana?

Jibu: Hayanajisiki kwa kufanya hivo. Bali inafaa kuyatumia kwa mujibu wa wanachuoni wote kama mfano wa Maalik, Abu Haniyfah, ash-Shaafi´iy na Ahmad. Ahmad ana mapokezi mengine ambapo anasema kuwa bado ni yenye kuendelea kutumiwa. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/46)
  • Imechapishwa: 19/11/2017