Swali: Unasemaje kwa yale yanayofanywa na baadhi ya vijana katika watoto wa waislamu hii leo ambapo wanavaa jezi za mazoezi zilizo ima na nembo za nchi za kikafiri, baadhi ya wachezaji mpira makafiri au ziko na nembo zilizo na kasumba kwa baadhi ya vyama vya mazoezi vya makafiri kwa kuwapenda. Je, huku ni katika kuwapenda makafiri?

Jibu: Kufanya hivi kunaweza kuwa sio katika kuwapenda makafiri kwa dhahiri. Lakini mwenye kufanya hivi katika moyo wake kuna kuwaadhimisha makafiri, kitu ambacho kinakinzana ima na asli ya imani au ukamilifu wake.

Lililo la wajibu kwa sisi waislamu ni kususa mavazi kama haya na tusiyanunue. Katika vile alivyotuhalalishia Allaah kuna ya kutosheleza. Kwa sababu tukivaa mavazi haya kuna kuwatukuza makafiri kwa njia ya kwamba tunajifakhari kwa kule kuvaa aidha picha au majina yao. Wao pia wanajifakhari kwa hili na wanaona kuwa ni kuwatukuza na kuwaheshimisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (02)
  • Imechapishwa: 02/05/2020