Majaaz katika Qur-aan


Swali: Je, katika Qur-aan kuna Majaaz?

Jibu: Katika Qur-aan hakuna Majaaz. Qur-aan yote ni ukweli na Sunnah vivyo hivyo. Kadhalika lugha kwa mujibu wa maoni sahihi kama walivyothibitisha hilo wanachuoni kama Shaykh-ul-Islaam, Ibn-ul-Qayyim na wengineo. Hata wale maimamu wane hakuna aliyesema hivo. Ijapokuwa baadhi yao wanaweza kukutana na neno kutoka kwa Imaam Ahmad ambapo wakasema Majaaz. Lakini hata hivyo hawamaanishi Majaaz yanayomaanishwa na hawa waliokuja nyuma. Wanachomaanisha ni yale Majaaz yanayojuzu. Majaaz haya ni kitu kilichozuliwa katika lugha na kimekuja baada ya maimamu wane.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 07/05/2018