Maiti wa kike anaombewa du´aa ya kupewa mume bora kama ilivyo kwa mwanamme?

Swali: Ikiwa jeneza ni la mwanamke wakati wa kumuombea du´aa mtu asome:

اللهم أبدلها زوجًا خيرًا من زوجها

“Ee Allaah! Mbadilishie mume bora kuliko mume wake.”

au du´aa hii ni yenye kukomeka kwa mwanamme peke yake?

Jibu: Anaweza kuombewa zile du´aa zilizopokelewa kwa njia iliyoenea:

“Ee Allaah! Mfanyie atayoyakuta Kwako mwanamke huyu ni bora kuliko aliyokuwemo.”

Kwa sababu maoni yenye nguvu katika maoni ya wanachuoni ni kwamba mwanamke anapokufa anakuwa bado yuko katika dhimma ya mume. Wakikusanyika Peponi basi atakuwa ni mke wa mume wake duniani. Lakini mume akifariki na mke baadaye akaolewa, wako waliosema kuwa atakuwa na yule mume mbora zaidi kitabia. Lakini maiti anatakiwa kuombewa du´aa ya jamaa na makazi. Muhimu kuliko yote mwanamke aombewe Allaah kumsamehe, amkunjulie kaburi lake na amfanyie wepesi.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=7gEAXZ3mkg8
  • Imechapishwa: 20/04/2020