Swali: Kuna mwanamke amekufa na ameandika katika wasia wake kwamba anataka aswaliwe katika Msikiti mtakatifu wa Makkah na sisi tunaishi Riyaadhw. Je, ni lazima kwetu kutekeleza wasia huu?
Jibu: Hapana. Sio lazima kutekeleza wasia huu. Miji ya Waislamu yote ni sawa na himdi zote ni Zake Allaah. Aswaliwe pamoja na Waislamu katika mji ambapo amekufa ndani yake.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (49) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-5-13.mp3
- Imechapishwa: 16/11/2014