Maiti ameacha anausiwa kujengewa kuba

Swali 108: Kuna mtu ameacha anausia kuweka kuba juu ya kaburi lake. Je, wasia wake utekelezwe?

Jibu: Wasia wake usitekelezwe. Ni wasia batili. Ni mwenye kupata dhambi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuzua katika amri yetu hii yasiyokuwemo basi atarudishiwa mwenyewe.”

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 119
  • Imechapishwa: 28/09/2019