Maiti aliyekufa Ramadhaan anatolewa Zakaat-ul-Fitwr?


Swali: Ikiwa wakazi wa nyumba ni watu nane ambao wote wamefunga Ramadhaan mpaka tarehe 27. Kabla ya mwezi kuisha mmoja katika wao akafa. Je, inajuzu kwa baba mwenye nyumba kumtolea Zakaat-ul-Fitwr?

Jibu: Sio wajibu kwake kumtolea Zakaat-ul-Fitwr kwa sababu amekufa kabla ya wakati uliyowajibishwa.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/368)
  • Imechapishwa: 23/06/2017