Swali: Uliishi pamoja na Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) ambaye alikuwa ni mmoja katika maimamu wakubwa wa leo. Tulikuwa tunapendelea kusikia kitu kidogo kuhusu maisha ya imamu huyu?

Jibu: Maisha ya imamu huyu sio kitu kipya kwenu. Mlikutana nacho. Maisha ya Imaam ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) yanaendana na maimamu wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah waliokuwa kabla yake. Ilikuwa ni maisha yaliyojengwa juu ya elimu, uelewa wa dini ya Allaah, kusoma chini ya wanachuoni, hamu kubwa ya elimu ya Hadiyth na ya Sunnah. Haya ndio yalikuwa maisha ya Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqiyqatu Da´wat-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/02011436.mp3
  • Imechapishwa: 27/08/2020