Swali: Ni ipi hukumu ya mahusiano kati ya jinsia mbili tofauti pamoja na kuzingatia kuwa dhamira ni nzuri na sio mbaya?

Jibu: Ni lazima kwa mwanamme kutokutana na mwanamke ambaye ni wa kwando kwake. Ni lazima kwake kujihadhari asiwe chemba na mwanamke, wasifanye makutano na maongezi yoyote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamme hatokuwa chemba na mwanamke isipokuwa watatu wao atakuwa ni shaytwaan.”[1]

“Tahadharini kuingia [maeneo walipo] kwa wanawake.” Kukasemwa: “Unasemaje juu ya shemeji?” Akasema: “Shemeji ni kifo.”[2]

Allaah (Ta´ala) amesema kuwaambia wakeze Mtume:

 فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ

“Msilainishe kauli asije akaingiwa na tamaa yule ambaye moyoni mwake mna maradhi.” (33:32)

Kinachotakiwa mwanamme awe na msimamo na ajiepushe kuzungumza na wanawake. Maongezi yanaweza kupelekea katika kilicho kibaya zaidi. Shaytwaan hutembea ndani ya mwanadani kama inavyotembea damu ndani ya mishipa. Kufunga njia za shari ni miongoni sababu za usalama kwa tawfiyq ya Allaah. Anayejifungulia juu ya nafsi yake mlango wa shari basi kunakhofiwa akatumbukia ndani yake isipokuwa yule aliyekingwa na Allaah. Tunamwomba Allaah hifadhi na uongofu.

[1] an-Nasaa´iy (4083) na Ahmad (02/339).

[2] al-Bukhaariy (5232), Muslim (2172), at-Tirmidhiy (1171), Ahmad (04/149) na ad-Daarimiy (2642).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-العلاقة-بين-الجنسين
  • Imechapishwa: 12/06/2022