Mahari ya bikira na asiyekuwa bikira


Swali: Ni yapi mahari ya Kishari´ah kwa msichana ambaye hajaolewa na mwanamke ambaye kishatalikiwa?

Jibu: Mahari hayana mpaka maalumu. Hakukutengwa mahari maalumu kwa yule ambaye hajaolewa, ambaye katalikiwa wala yule ambaye kafiwa. Atayowekea hata kama yatakuwa ni madogo, yatosha. Sawa mwanamke huyo alikuwa ni bikira hajaolewa, alikuwa amekatalikiwa au alikuwa amefiwa. Watayopatana mwanaume na mwanamke yanatosha, sawa yakiwa madogo au yakiwa mengi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 22/03/2018