Magomvi ya wanandoa hayatakiwi kufikia kiasi hichi


Swali: Wakati fulani mume na mke wanagombana ambapo mume anamsusa kitandani, hamzungumzishi na anapoingia nyumbani hamtolei salamu. Je, kitendo hichi kinaafikiana na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kususa? Ni upi mwenendo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa mke wake wakati wa magomvi?

Jibu: Haya ni makosa hali za wanandoa kufikia kiasi hichi akamsusa kitandani na katika mazungumzo. Ni kosa kubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mbora wenu ni yule mbora kwa ahli zake na mimi ni mbora kwa ahli zangu.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), nyumbani kwake, alikuwa akisaidia kazi za nyumbani. Kunapofika wakati wa swalah anatoka kwa ajili ya swalah.

Haifai kwa mtu akamsusa mke wake hata kama atakosea. Astahamili na avute subira. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muumini wa kiume asimchukie muumini wa kike. Akichukia kutoka kwake tabia fulani ataridhia nyingine.”

Amesema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Wanawake wameumbwa na ubavu uliopinda. Kilichopinda zaidi ni kile cha juu; ukienda kukinyoosha utakivunja na ukistarehe naye utastarehe naye akiwa ni mwenye kupinda.”

Mambo haya ya kususa hayazidishi chochote isipokuwa matatizo. Ni lazima kwake kusubiri, kustahamili, amfanyie upole mke na amzungumzishe kwa kiasi cha akili yake hadi mambo yawe sawa.

Inatosha kwa mke kumfanyia tabasamu tu. Tabasamu yako inaondosha kila kilichomo moyoni mwake. Kinyume na hayo kuvimbisha kwako uso kunamkimbiza. Kwa hiyo mtu azichunge hali hizi ili aweze kuishi na mke wake maisha mazuri na yenye furaha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (76) http://binothaimeen.net/content/1756