Magazeti yasiyotakiwa kutupwa hovyo


Swali: Je, inafaa kuyatumia magazeti kama meza ya kulia? Ikiwa haijuzu tuyafanye nini baada ya kuyasoma?

Jibu: Haijuzu kuyatumia magazeti kama meza ya kula juu yake, kuyafanya ni faili za mahitajio mbalimbali wala kuyatweza kwa sampuli mbalimbali ikiwa ndani yake kumeandikwa baadhi ya Aayah za Qur-aan au utajo wa Allaah. Ikiwa hali ndio hiyo tuliyoitaja basi lililo la wajibu ni kuyahifadhi mahali ambapo ni munasibu, kuyachoma moto au kuyazika chini ya udongo msafi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/439)
  • Imechapishwa: 24/02/2021