Magazeti na makala zinazoeneza picha za wanawake walio uchi

Swali: Kuna baadhi ya magazeti yanayoenea picha za wanawake walio uchi au makala yanayoupiga vita Uislamu. Je, inajuzu kuyauza?

Jibu: Haijuzu. Bali ni wajibu kuyachana. Magazeti ambayo ndani yake kuna mambo ya nyuchi, picha zinazofanana na mambo ya nyuchi, au vitabu vinavyoitia mashaka dini au vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah, vyote hivi ni wajibu kuvichana na kuvichoma. Haijuzu kuviuza. Isipokuwa kama mtu ataviuza kwa sababu ya kutaka kukemea, kuwafikishia wahusika au kuwaraddi wazushi. Katika hali hii ni sawa. Hili linamuhusu yule mwanafunzi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
  • Imechapishwa: 04/03/2018