Mafundisho au uongozi kwa ajili ya pesa

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu anayeadhini kwa ajili tu ya mshahara?

Jibu: Mosi inapaswa kutambulika kwamba bonasi ambayo serikali inatoa kuwapa maimamu na waadhini sio mshahara. Ni zawadi kutoka katika wizara ya mali kwenda kwa watu wanaonuwanufaisha waislamu, kama mfano wa waalimu, maimamu, waadhini, mahakimu na viongozi. Sio kwa lengo la mshahara mpaka tuseme kuwa haifai kupokea kwa mkabala wa ´ibaadah. Ni zawadi kutoka katika wizara ya fedha kwa anayefanya kazi hii.

Lakini inafaa kwa muadhini na imamu kuadhini au kuwaswalisha watu kwa ajili ya mshahara? Usiwe na nia hiyo. Nia kama hiyo inaporomosha kitendo. Katika hali hiyo hupati thawabu za adhaana, swalah, hukumu wala thawabu za kufundisha. Nuia kwamba unafundisha na kwamba unapokea kile unachopata kutoka serikalini ili uweze kukitumia katika mambo yako ya kidunia. Ukifanya hivo basi unakuwa ni mwenye kunufaika na pesa na nia yako njema.

Hata hivyo shaytwaan anaweza kumshinda mwanadamu na hivyo akaadhini au akafundisha kwa ajili ya zawadi hii. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema mtu kama huyo hana hapati chochote siku ya Qiyaamah. Amesema kweli. Huyu amepata malipo yake duniani. Tunatakiwa kuwahimiza watu juu ya kuzitengeneza nia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (20 A) Dakika: 13:27
  • Imechapishwa: 12/10/2021