Maelezo ya Hadiyth “Hakuna kinachorudisha Qadar nyuma ila du´aa”

Swali: Ni ipi maana ya kwamba hakuna kinachorudisha Qadar nyuma isipokuwa du´aa peke yake?

Jibu: Maana yake ni kwamba du´aa inaingia ndani ya Qadar. Allaah ameitundika Qadar juu ya du´aa. Du´aa na Qadar vyote viwili vimekadiriwa. Imekuja katika Hadiyth kwamba hukinzana na kimoja wapo chenye kuzidi nguvu kingine ndicho huchukua nafasi. Hivyo Qadar inakuwa imetundikwa juu ya kitu. Kwa mfano mtu akiwa ni mwenye kuwaunga ndugu zake basi hiyo inakuwa ni sababu ya kurefushiwa umri wake wa kuishi. Kuwaunga ndugu kunaingia ndani ya Qadar. Kwa njia ya kwamba Allaah anakuwa amekadiria kuwa mtu huyu umri wake utarefuka kwa kuwaunga ndugu zake. Upande mwingine amekadiria kuwa mtu huyu umri wake utapungua kwa kuwakata ndugu zake. Upande mmoja amekadiria kuwa mtu huyu atapata mambo haya kwa sababu ya kuomba du´aa. Upande wa pili amekadiria kuwa huyu hatopata yale ayaombayo kwa sababu ya kuacha kuomba du´aa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (07) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/434/434.mp3
  • Imechapishwa: 22/12/2018