Maelezo kuhusu Hadiyth “Mkono uliyo juu ni mbora kuliko mkono uliyo chini”

Swali: Ni ipi maana ya yale yaliyopokelewa?

“Mkono uliyo juu ni mbora kuliko mkono uliyo chini.”?

Jibu: Hadiyth hii ni Swahiyh. Mkono uliyo juu ni ule mkono wa mwenye kutoa. Mkono uliyo uliyo chini ni ule mkono wa mwenye kupokea. Kwa msemo mwingine yule mwenye kutoa yujuu kuliko yule mwenye kupokea. Kwa sababu yule mwenye kupokea anajiona yuchini kuliko yule mwenye kutoa na wakati huohuo yule mwenye kutoa anajiona yujuu kuliko yule mwenye kupokea. Kwa ajili hii utamuona yule mwenye kupokea ananyenyekea zaidi kuliko yule mwenye kutoa. Mkono uliyo juu ni ule mkono wa mwenye kutoa. Mkono uliyo uliyo chini ni ule mkono wa mwenye kupokea.

Haya ni mashaji´isho ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya kwamba mtu awe ni mwenye kuvipa nyongo vile vilivyoko kwa watu, asivikodolee macho na asivitazame. Midhali ni mwenye kivupuuza hatovipokea. Lakini ikiwa ni zawadi basi itambulike kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akipokea zawadi na akionyesha shukurani. Bali wakati ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) alipopewa zakaah kwa kazi ya kuitumikia na kuikusanya zakaah kutoka kwa wale ambao inawawajibikia ambapo akasema:

“Ee Mtume wa Allaah! Si uwape swadaqah hii wale wenye haja zaidi yangu.” Akamwambia: “Kile kitachokujia katika hali hii na wewe si mwenye kuipupia basi ipokee. Vinginevyo usiitabishe nafsi yako.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (44) http://binothaimeen.net/content/1022
  • Imechapishwa: 21/02/2019