Mu´tazilah wana utata katika kusema kuwa Maneno ya Allaah yameumbwa. Madhehebu haya yapo na yameenea leo katika baadhi ya miji. Madhehebu ya Ashaa´irah na Mu´tazilah yanasomeshwa leo katika baadhi ya miji ya kiarabu. Wana vitabu vingi. Wafasiri wengi leo wamekosea pia katika hili kama mfano wa Zamakhshariy na kitabu chake “al-Kashshaaf”. Kitabu hiki kimejengwa juu ya hili. al-Bulqiyniy amesema ametoa kwenye “al-Kashshaaf” makosa ya madhehebu ya Mu´tazilah ikiwa ni pamoja na alivosema wakati walipofasiri Aayah:

فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ

“Basi atakayewekwa mbali na Moto na akaingizwa Peponi kwa hakika amefuzu.” (03:175)

Akasema “Ni kufaulu kupi kuliko kukubwa kuliko Pepo?” Anachokusudia kwa kusema hivo ni kukanusha kuonekana kwa Allaah siku ya Qiyaamah.

Ikiwa vitabu vya Tafsiyr ya Qur-aan leo vina madhehebu ya Mu´tazilah, mwanafunzi anaweza kuvisoma na kuathirika na upotevu uliyomo. Kwa hiyo mwanafunzi anatakiwa kujua baadhi ya utata huu na jinsi ya kuziraddi. Ndio maana sisi tunasoma baadhi ya utata wao na kumjuza nao mwanafunzi na namna ya kuziraddi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/183)
  • Imechapishwa: 30/05/2020