Swali 29: Mwenye kuwakufurisha watawala na anawataka waislamu kuwafanyia uasi watawala wao – je, ni katika Khawaarij?

Jibu: Haya ndio madhehebu ya Khawaarij. Kama anaona kufaa kuwafanyia uasi watawala wa waislamu na baya zaidi kuliko hilo akawakufurisha, basi hayo ndio madhehebu ya Khawaarij.

Wale wanaowakufurisha watawala wa waislamu wote haya ndio Khawaarij wabaya zaidi. Kwa sababu hawakumbagua yeyote. Kuwahukumu watawala wote wa waislamu kwamba ni makafiri ni jambo baya kuliko hata madhehebu ya Khawaarij. Kwa sababu amewajumuisha wote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 141
  • Imechapishwa: 21/09/2019