Wanachuoni wametaja hekima ya kukatazwa kuwafanyia uasi watawala na wameifanyia utafiti kutoka katika maandiko. Hili ni lenye kuingia katika kanuni yenye kusema: kukipatikana madhara mawili ambayo hayawezi kuepukwa basi tunafanya madhara madogo ili kuepuka yale makubwa. Kadhalika kukipatikana manufaa mawili ambayo hayawezi kufanyika yote mawili, basi tunafanya manufaa makubwa hata kama yale madogo yatapita. Kwa mfano katika kufanya uasi kwa watawala kunapatikana madhara mengi ikiwa ni pamoja na; vurugu, mfarakano, kutofautiana, chuki, malalamiko, kumwagika kwa damu, watu kugawanyika na mioyo yao kutofautiana, waislamu kushindwa na utukufu wa nchi kuondoka na hivyo maadui wanatapa kuwageukia mgeuko muovu juu yao, maadui wanapata kuingia, kunatokea fujo, kukosekana amani, bali kukosekana uhai kabisa, uhai wa siasa kutikisika, uhai wa kuichumi kutikisika, uhai wa kibiashara kutikisika na uhai wa kimafunzo kutikisika, hutokea fitina yenye kumkumba aliyepo na asiyekuwepo. Haya ni madhara makubwa mno. Ikiwa mtawala amefanya maovu; kama kuwadhulumu baadhi ya watu, kuwatia jela, akanywa pombe, akasimamia baadhi ya mali kwa kuwadhulumu baadhi ya watu, haya ni madhara madogo. Inatakiwa kwa waislamu wastahamili mahala popote na haijalishi ni wakati gani yatatokea hayo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (02/553)
  • Imechapishwa: 19/05/2020