Swali: Je, mtu anaweza kusema wanawake kupanda juu ya vipando kunatolea dalili kuonesha kuwa inajuzu kwao kuendesha gari?

Jibu: Hakuna ukhatari wa kupanda mnyama. Hakupelekei katika madhara. Hilo ni tofauti na mwanamke kuendesha gari. Hilo linapelekea katika madhara na khatari. Hilo lina madhara mengi. Kwa ajili hiyo ndio maana haitakiwi kwake kuendesha. Mwanamke akimiliki gari na akawa na ufunguo wa gari anakuwa ni mwenye kwenda kwa anayemtaka na wakati anapotaka. Yuko na ufunguo wa gari yake na hakuna yeyote wa kumzuia. Mwanaume hawezi kufanya lolote. Mtenda dhambi anaweza kuwasiliana naye na kupanga naye miadi. Ni kipi chenye kumzuia kuchukua ufunguo wa gari, kuwasha na kwenda zake kwenye miadi? Kwa kuwa ni mwenye kuchukua zake uhuru wake [sauti imekatika]…

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-02.mp3
  • Imechapishwa: 06/06/2018