Madhara ya kutotekeleza nadhiri baada ya kuiweka

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuweka nadhiri na akasema:

“Haiji kwa kheri. Haitoki isipokuwa kwa aliye bakhili.”

Ni wingi ulioje wa watu ambao wanaweka nadhiri na wala hawatekelezi. Kutotimiza nadhiri midhali nadhiri hiyo ni njema ni jambo lina matokeo mabaya. Amesema (Ta´ala):

وَمِنْهُم مَّنْ عَاهَدَ اللَّـهَ لَئِنْ آتَانَا مِن فَضْلِهِ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ الصَّالِحِينَ فَلَمَّا آتَاهُم مِّن فَضْلِهِ بَخِلُوا بِهِ

“Miongoni mwao wako waliomuahidi Allaah [kwamba]: “Akitupa katika fadhila Zake, basi bila shaka tutatoa swadaqah na tutakuwa miongoni mwa waja wema.” Alipowapa katika fadhila Zake, walizifanyia ubakhili.”[1]

 Hawakusema kweli:

وَتَوَلَّوا وَّهُم مُّعْرِضُونَ

“… na wakakengeuka na huku wakipuuza.”[2]

 Hawakuwa katika wema:

فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِي قُلُوبِهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ يَلْقَوْنَهُ بِمَا أَخْلَفُوا اللَّـهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ

“Basi akawapachika unafiki katika nyoyo zao mpaka siku watakayokutana Naye kwa vile walivyomkhalifu kwao Allaah kwa waliyomuahidi na kwa yale waliyokuwa wakikadhibisha.”[3]

Haya matokeo mabaya. Allaah akaweka unafiki katika nyoyo mpaka wakati wa kufa. Kwa sababu hawakutimiza ahadi.

Ikiwa nadhiri imekatazwa na matokeo yake yanaweza kuwa mabaya basi muumini aliye na busara haweki nadhiri. Ikiwa Allaah amekuweka katika hali ya usalama basi uko katika hali ya usalama bila kuweka nadhiri. Ikiwa Allaah amekuidhini hali ya usalama basi usiweke nadhiri.

[1] 09:75-76

[2] 09:76

[3] 09:77

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (36) http://binothaimeen.net/content/801
  • Imechapishwa: 18/03/2018