Swali: Katika hizi siku kumi za mwisho kunaenezwa nyujumbe kwa njia ya simu zinazosema kwamba watu wameota usiku wa Qadr. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Nyuma ya simu wamejificha watu madajali. Wanachotaka ni kuwashawishi watu. Usikubali kitu chochote kutoka katika simu. Elimu ipo. Wanachuoni wapo. Vitabu aminifu vipo. Tunarejea huko. Kuhusu madajali hawa ambao wamejificha nyuma ya simu malengo yao ni kutaka kuwapotosha watu na kuwashughulisha watu na mambo haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13445
  • Imechapishwa: 14/05/2020