Madai ya kwamba baadhi ya miji inaswali Fajr kabla ya wakati

Swali: Katika mji wangu wanaswali Subh kabla ya wakati wake. Nifanye nini kwa kuzingatia ya kwamba endapo nitaswali nao sintoweza kuwakataza?

Jibu: Huna uhakika juu ya hili. Mimi sidhani waislamu wote katika mji watakubaliana juu ya kuswali kabla ya wakati. Kumedhihiri tabia kwa baadhi ya vijana ambapo wanasema kuwa leo waislamu wanaswali Fajr kabla ya wakati wake. Hivi kweli waislamu [wote] watakusanyika katika makosa na upotevu? Haya ni maneno ya wajinga na sio maneno ya wenye akili wala ya wanachuoni. Swali pamoja na waislamu wenzako na himdi zote ni za Allaah. Achana na mambo ya mashaka. Lau ingelikuwa kwa mfano ni mtu mmoja au kundi fulani wanaweza kukosea. Lakini nchi nzima na watu wote wanaswali na kusema kuwa wanakosea! Hili si sahihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14819
  • Imechapishwa: 28/06/2020