Machukizo ya kuswali maeneo palipo na picha

Swali: Ni ipi hukumu mtu akiswali nyumbani kwake na maeneo anaposwali kukawa kuna majarida au magazeti yaliyo na picha zinazoonekana juu ya madawati, mazuliwa na mfano wake?

Jibu: Kilicho cha lazima kwa muislamu ni yeye kuswali mkusanyiko msikitini na wala asiswali peke yake au nyumbani kwake isipokuwa kutokana na udhuru unaokubalika katika Shari´ah unaomjuzishia yeye kufanya hivo. Inachukiza kuzielekea picha na kuswali mahali kulipo na picha zilizotundikwa juu ya ukuta. Ikiwa picha zimetandikwa chini basi ni zenye kutwezwa.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdul-´Aziyz Aalus-Shaykh

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (20583)
  • Imechapishwa: 14/05/2022