19Kamwe usilale na mwanamke awapo mwezini. 20Kamwe usilale na mke wa jirani yako na hivyo kujitia mwenyewe najisi naye. 21Kamwe usimtoe mtoto wako yeyote kuwa sadaka kwa mungu Moleki maana kufanya hivyo utalikufuru jina langu mimi Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. 22Kamwe usilale na mwanamume mwenzio kana kwamba ni mwanamke. Hilo ni chukizo. 23Kamwe usilale na mnyama ili usijitie najisi; mwanamume au mwanamke yeyote kamwe asifanye hivyo; kufanya hivyo ni upotovu.

24Msijitie najisi kwa kufanya mambo hayo kwani kwa sababu ya mambo hayo nayafukuza mataifa yaliyo mbele yenu kwa vile wao hufanya hayo na kujitia najisi. 25Nchi yao ilitiwa unajisi nami nikaiadhibu, nayo ikawakataa wakazi wake. 26Lakini nyinyi na wageni wanaokaa kati yenu ni lazima kuyashika masharti na maagizo yangu na wala msifanye machukizo hayo. 27Machukizo hayo waliyafanya watu waliokaa katika nchi ya Kanaani kabla yenu, nao wakaitia nchi unajisi. 28Basi, nyinyi msifanye mambo hayo, la sivyo nchi hiyo itawatapika kama ilivyolitapika taifa lililokuwa kabla yenu. 29Watu wote watakaofanya mambo hayo ya kuchukiza ni lazima watengwe mbali na watu wao. 30Kwa hiyo shikeni kikamilifu yote ninayowaagiza; msifuate mazoea yoyote ya kuchukiza yaliyofanywa na wale walioishi nchini kabla yenu, msije mkajitia unajisi kwayo. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.”

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Walawi 18:19