Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anakusudia nini wakati alipomkataza mwanamke kuvua nguo zake nje ya nyumbani kwake? Inafaa kwa mwanamke ambaye siku zote amelazimiana na Hijaab kutoka na kwenda katika nyumba za starehe za wanawake kuogelea na wanawake wenzake kuvua nguo zake?

Jibu: Mwanamke haifai kwake kuogelea na wanawake. Haitakiwi kwa wanawake kutazamana wakati wanapoogelea. Ni fitina. Fitina inatokea kwa wanawake kati yao. Haijuzu jambo hili. Anaweza tu kuogelea katika pahala patupu. Hata hivyo mabwawa ya wanawake hayajuzu. Yana fitina, ukosefu wa haya na makatazo mengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340126_0.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020