Mabachala kutumia dawa za kupunguza matamanio

Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia madawa yanayopunguza kuja kwa matamanio pamoja na kuzingatia kwamba yanakuwa mengi kwa wale ambao ni mabachala wasiokuwa na uwezo wa kuoa?

Jibu: Hili linategemea ushauri wa daktari. Ikiwa kuyatumia madawa haya hayamdhuru mtu katika siku za huko mbeleni, hakuna neno. Ama ikiwa yanamdhuru hayafai. Kila kitu kinachomdhuru mtu basi kimekatazwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna madhara wala kudhuriana.”

Mtu anahitajia nguvu hizi huko mbeleni. Mtu atakapooa atazihitajia na atatamani abaki nayo hali ya kuyachunga mpaka pale utapokuja wakati ambao Allaah atamsahilishia mke na mambo yakawa mepesi. Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaelekeza vijana katika jambo pindi aliposema:

“Enyi kongamano la mabarobaro! Yule miongoni mwenu atakayeweza kuoa basi na aoe. Kwani hilo litamfanya kuteremsha macho na kuhidhi utupu. Asiyeweza basi afunge. Kwani hiyo kwake ni kinga”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (51) http://binothaimeen.net/content/1159
  • Imechapishwa: 30/06/2019