Maandamano yameharamishwa na Uislamu

Swali: Ni ipi hukumu ya migomo na maandamano? Je, ni mambo yana mtazamo fulani katika dini? Kuna baadhi ya wanachuoni wamefutu ya kwamba ni katika aina kubwa kabisa ya kupigana Jihaad katika njia ya Allaah dhidi ya madhalimu.

Jibu: Huyu ni muongo. Mwenye kusema kuwa ni katika Jihaad ni muongo. Maandamano sio katika Jihaad. Ni miongoni mwa mambo yanayoharamishwa na Uislamu kutokana na madhara yanayopatikana ndani yake. Kuna maasi ya kumuasi mtawala, vurugu, kumwaga damu, uharibifu na kadhalika. Kuna madhara tele. Isitoshe sio katika dini ya Uislamu. Hizi ni nidhamu za kimagharibi. Hizi sio nidhamu za waislamu. Kuhusu waislamu wao wanatanguliza utulivu, utaratibu na kutatua matatizo kwa mujibu wa Shari´ah na sio kwa kufanya maandamano na migomo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13398
  • Imechapishwa: 26/04/2018