Swali: Wako wanaosema kuwa haijuzu kuitumia Hadiyth inayowahusu Khawaarij kwa wale waaotoka nje hii leo katika maandamano dhidi ya mtawala fulani na kwamba maandamano haya ni ya amani na kwamba hakuna wengine wanaoyakataza isipokuwa Ahl-ul-Bid´ah peke yao.

Jibu: Maandamano sio katika Uislamu kutokana na ile shari inayopelekea. Mfano wa hilo ni kufarikisha umoja wa waislamu kukiwemo uharibifu na umwagaji damu. Maandamano sio ufumbuzi sahihi. Ufumbuzi unakuwa kwa kufuata Qur-aan na Sunnah. Yaliyopitika hapo kale ni makubwa zaidi kuliko shari ilioko hii leo. Lakini hata hivyo yanatakiwa kutatuliwa kwa mujibu wa Shari´ah na si kwa mujibu wa mipango ya makafiri na maandamano yaliyotolewa huko nje. Haya sio katika Uislamu. Fujo sio katika Uislamu. Uislamu unahimiza katika marekebisho, subira, hekima na kuyarudisha mambo kwa wanachuoni:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ

“Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho.”[1]

[1] 04:59

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ls–1434011.mp3
  • Imechapishwa: 21/03/2021