Swali la kwanza: Je, maandamano na mgomo ni katika Jihaad?

Imaam Ibn Baaz: Hapana! Hili ni makosa, ni makosa, ni makosa! Hii ni fitina na shari. Haijuzu!

Swali la pili: Je, maandamano ya wanaume na wanawake dhidi ya mtawala na kiongozi ni katika njia za kufanya Da´wah? Na kwa yule atakayekufa katika hali hii kafa shahidi katika njia ya Allaah?

Imaam Ibn Baaz: Sionelei kama maandamano ya wanaume na wanawake ndio ufumbuzi. Bali hili linasababisha matatizo mengi, maovu, na baadhi ya watu wanaonewa, na wengine wanaonewa pasi na haki yoyote.

Lakini kununi za Kishari´ah ni kuandikiana, kupeana nasaha na kusaidiana katika kheri. Yatendeke katika hali nzuri. Katika hali hii wasogelewe wanachuoni, Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale wanaowafuata kwa wema. Kuandikiane na pawepo mazungumzo ya kupeana nasaha kwa wale waliyokosea, watawala, wafalme na viongozi. Yote haya yatendeke bila ya kutangaza hadharani katika mimbari – huyu kafanya hivi na vile na mfano wa hayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=B9IMyUksKrw
  • Imechapishwa: 05/09/2020