Maandamano ili kupiga vita sheria za binaadamu


Swali: Ni ipi hukumu ya kujiunga na makundi ya Kiislamu ili kupiga vita sheria za watu?

Jibu: Hili ni wajibu. Ni swali?

Swali: Ni ipi hukumu ya kujiunga na makundi ya Kiislamu ili kupiga vita kanuni?

al-Albaaniy: Ikiwa unarudilia swali baada ya kukwambia kwamba ni wajibu, nadhani kuwa ni lazima uwe na fikira nyuma ya hilo. Una maanisha nini kwa neno “kujiunga”?

Swali: Uasi.

al-Albaaniy: Allaah akuongoze. Ni namna hii mtu huuliza swali? Uasi una maanisha maandamano, si ndio?

Muulizaji: Ndio.

al-Albaaniy: Inaonekana kwamba hukuwa pamoja na sisi karibuni. Tulizungumzia kwa utafiti mrefu na hatimae tukafikia ya kwamba maandamano haya yanayofanywa ili kukataza kitu katika kanuni iliyowekwa, kwamba ni desturi ya makafiri na wala haijuzu kwa waislamu kuifuata.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.ibnbaz.se/Artiklarna/601-700/072.html
  • Imechapishwa: 05/09/2020