Swali: Kuna wanaosema kuwa maandamano dhidi ya watawala wa kikafiri yanajuzu, kwa kuwa kafiri inajuzu kufanya uasi kwake?

Jibu: Maandamano ikiwa yatapelekea katika madhara, uharibifu, umwagikaji wa damu na kukosekana amani hayajuzu. Na kuwasimamia watawala wa kikafiri haiwi kwa maandamano. Inakuwa kwa Jihaad katika njia ya Allaah chini ya uongozi wa Kiislamu utao ongoza watu na kuwapiga vita makafiri. Kama ilivyokuwa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake. Waliwashambulia makafiri na majeshi chini ya uongozi wa Kiislamu chini ya uongozi uliopangwa. Wakawapiga vita. Ama maandamano haya hayaji ila kwa shari. Na wala hayaleti kheri bali inakuwa ni sababu ya fitina na wala hayaleti faida ya kitu. Kama mnavyoona leo. Je, maandamano ya leo yameleta kheri? Hayakuleta kheri na wala hayaishi baada ya maandamano kunajitokeza mengine. Kwa kuwa hayakuandaliwa Kishari´ah na chini ya uongozi na mashambulizi ya Kiislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda: as-Salafiyyah haqiyqatuhaa wa simaatuhaa
  • Imechapishwa: 06/09/2020