Swali: Ni nini maana ya Wahdat-ul-Wujuud?

Jibu: Ni kundi au kwa msemo mwingine Suufiyyuun waliopetuka mipaka wamefikia kiwango cha kuamini ya kwamba kila tunachokiona, tunachokigusa, tunachokisikia na tunachokihisi, vyote hivyo ni Allaah. Hii – na tunaomba kinga kwa Allaah – ni aina mbaya kabisa ya ukafiri. Bali heunda yule anayepinga kuwepo kwa Allaah akawa ni bora kuliko yule anayeamini imani ya Wahdat-ul-Wujuud. Tunamuomba Allaah afya na usalama.

Wahdat-ul-Wujuud ina maana ya kwamba mti, jibali, vyoo, wanyama, vijibwa na kila tunachoona na kusikia ni Allaah. Haya yamesemwa na wengi katika wale ambao wameathirika na Suufiyyah. Hawa ni wale ambao Hizbiyyuun wanadai kuwa ndio viongozi wao, kama Sayyid Qutwub wakati alipofasiri “Suurat-ul-Ikhlaasw” kwa tafsiri ya Wahdat-ul-Wujuud na kadhalika Hasan al-Bannaa. Ni msiba mkubwa ulioje kushinda msiba huu kuwafanya watu kama hawa ndio vingozi wa kuigwa na kufuatwa na mtu ikaachwa Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alnajmi.net/voices.php?action=show&id=155
  • Imechapishwa: 26/08/2020