´Ibaadah ni neno lililojumuisha kila kile anachokipenda Allaah na kukiridhia, miogoni mwa maneno na vitendo, sawa vya dhahiri na vilivyojificha. Vilevile ni kila amri iliyoamrishwa au kukatazwa na Shari´ah. Kila amri iliyoamrishwa na Shari´ah, sawa ikiwa ni maamrisho kwa njia ya uwajibu au mapendekezo, basi ni wajibu kuitekeleza. Kila katazo lililokatazwa, sawa kwa njia ya uharamu au utakaso, ni lazima kujiepusha nalo. Hii ndio ´ibaadah. Ni kumtii Allaah na kumtakasia nia.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/45)
  • Imechapishwa: 07/06/2020