Maana ya Muwaalaah kwa mujibu wa al-Fawzaan


Swali: Allaah (Ta´ala) Amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ

“Enyi mlioamini! Msiwachukuwe Mayahudi na Manaswara [kuwa ndio] marafiki walinzi. Wao kwa wao ni marafiki walinzi. Na yeyote atakayewafanya marafiki; basi hakika yeye ni miongoni mwao.” (05:51)

Ni nini maana ya Muwaalaah katika Aayah hii? Ni lini Muwaalaah inakuwa kufuru kubwa?

Jibu: Muwaalaah ni kuwapenda, kuwanusuru na kuwasaidia dhidi ya Waislamu. Hii ndio Muwaalaah. Ni kuwapenda ndani ya moyo, kuwanusuru na kuwasaidia dhidi ya Waislamu. Vilevile pamoja na kuwatapa na kuwasifu. Yote haya yanaingia katika neno Muwaalaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ww.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_13.mp3
  • Imechapishwa: 19/06/2018