Swali: Ni vipi mtu atajua kuwa kitendo ni ususuwavu na sio cha Kishari´ah? Kuna watu ambao wanasema kuwa mwenye kuachia ndevu na kupandisha nguo zake amefanya ususuwavu.

Jibu: Kuwa na ususuwavu ni kuzidisha kile kiwango kilichowekwa katika Shari´ah. Hii ndio maana ya ususuwavu. Hata hivyo kushikamana na kiwango kilichowekwa katika Shari´ah ndio haki.

Nguo zinatakiwa kwenda mpaka kwenye tindi za miguu. Hapa ndio mpaka wa mwisho. Chenye kuvuka chini ya tindi mbili za miguu ni Motoni, hivyo ndivyo alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Katika suala hili mtu anatakiwa afuate desturi ya watu wa mji. Ikiwa wanavaa mpaka kwenye tindi za miguu, nawe vaa mpaka kwenye tindi za miguu. Usende kinyume nao. Itakuwa ni kutaka kisuonekana ukiende kinyume na watu wa mji. Ukienda kinyume nao kwa kitu kilichoruhusiwa utakuwa umefanya ususuwavu katika suala hili. Na ikiwa wanavaa hadi katikati ya muundi, nawe vaa hadi katikati ya muundi na fuata desturi ya mji.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (40) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatsah%20%20-%2028%20-%2012%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017