Maana ya kumuona kwa moyo


Swali: Wanachuoni (Rahimahumu Allaah)  wanasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona Mola wake kwa moyo wake. Nini wanachokusudia?

Jibu: Hapa ni pale alipopandishwa mbinguni. Wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipopandishwa mbinguni na akavuka mbingu ya saba mpaka mkunazi wa mwisho, wapo wanachuoni waliosema kuwa alimuona Mola wake kwa macho yake. Wengine wakasema kuwa alimuona kwa moyo wake na si kwa macho yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (107) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatoulahfan-22-06-1441.mp3
  • Imechapishwa: 04/09/2020