Maana ya kuifanya Qur-aan (جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا)

Swali: Nini maana ya ´kufanya` katika maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا

“Hakika Sisi tumefanya Qur-aan ya Kiarabu.”? (43:03)

Jibu: Tumeisahilisha. Mu´tazilah wanasema:

إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا

“Hakika Sisi tumefanya Qur-aan ya Kiarabu.”

bi maana tumeiumba. Ndio maana wanasema kuwa Qur-aan imeumbwa. Maana yake sahihi ni kwamba Allaah ameiwepesisha kwa lugha ya kiarabu. Kwa msemo mwingine ameiteremsha Qur-aan kwa kiarabu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qaa´idah al-Marraakushiyyah (02)
  • Imechapishwa: 30/04/2020