Maana ya kudhihirisha dini katika miji ya kikafiri


Swali: Leo kuna miji ya kikafiri watu wanaishi na muislamu hakandamizwi wakati wa kutekeleza kwake alama za dini. Je, katika hali hii ni wajibu kufanya Hijrah kuhama kutoka katika miji hiyo?

Jibu: Ndio, akiwa ana uwezo ni wajibu kwake kufanya Hijrah. Kwa sababu hawezi kulingania katika Tawhiyd na kukataza shirki.

Tunapozungumzia “kudhihirisha dini” haihusiani na yeye kuswali tu na kufunga na hawamkandamizi. Kudhihirisha dini ina maana kulingania katika dini ya Allaah kwa kuita katika Allaah kupwekeshwa na kukataza Shirki na kuamrisha mema na kukataza maovu. Hii ndio maana ya kudhihirisha dini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (43) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-03-17.MP3
  • Imechapishwa: 16/11/2014