Maana ya kijakazi kumzaa bibi yake

Swali: Imepokelewa katika Hadiyth kupitia kwa ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Miongoni mwa alama za Qiyaamah ni kijakazi kumzaa bibi yake.”

Naomba unifafanulie na unibainishie maana ya kijakazi kumzaa bibi yake?

Jibu: Maana yake ni kwamba miongoni mwa alama za Qiyaamah ni masuria watakuwa wengi kati ya watu mpaka kijakazi amzae bibi yake. Bi maana kijakazi atabeba mimba kutoka kwa bwana wake na hivyo amzae bibi yake. Kwa sababu mtoto wa bwana anakuwa bibi na mtoto wa bwana naye anakuwa bwana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/496)
  • Imechapishwa: 12/03/2021