Maana ya adhaana na ni lazima kuitikia?

Swali: Je, adhaana ni matangazo na ulazima?

Jibu: Ndio. Adhaana ni matangazo ya kuingia kwa wakati na wito wa swalah. Ni lazima adhaana iitikiwe.

حي على الصلاة، حي على الفلاح

“Njooni katika swalah, njooni katika mafanikio.”

Huu ni wito. Maana ya حيَّ elekeeni katika swalah na elekeeni katika mafanikio. Kwa ajili hiyo alipokuja bwana mmoja kipofu kwa Mtume mtukufu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: “Ee Mtume wa Allaah! Sina kiongozi wa kuniongoza msikitini. Je, ninayo ruhusa ya kuswali nyumbani kwangu?” Akampa ruhusa kisha baadaye akamuuliza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Je, wasikia wito wa swalah?” Akasema: “Ndio.” Akasema: “Basi imewajibika.” Kwa hiyo kuitikia ni lazima la lazima kwa wanamme wote ambao ´ibaadah ni yenye kuwawajibikia. Isipokuwa kukiwepo udhuru kama mfano wa mgonjwa, mwenye kuogopa, anayechunga mali anachelea itapotea endapo ataitikia na mfano wao ambao wanazuoni wamebainisha wenye udhuru ya kuacha swalah ya ijumaa na swalah ya mkusanyiko.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdil-´Aziyz bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3992/ما-معنى-ان-الاذان-هو-اعلان-والزام
  • Imechapishwa: 04/06/2022